10/13/2020

Konde Boy Atangaza Hali ya HatariKINARA wa pasi za mwisho kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu na nyota wa klabu ya Simba, Luis Miquissone ‘Konde Boy’ amesema kuwa achana na alichokifanya kwenye michezo mitano iliyopita kwani amejipanga kuuwasha moto mkali zaidi pale ligi itakaporejea baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa.

Luis amekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu ambapo amehusika kwenye mabao sita kati ya 14 ambayo Simba imefunga kwenye michezo yao mitano iliyopita.

Akizungumzia kiwango chake Luis alisema: “Namshukuru Mungu kwa kuwa na mwanzo mzuri msimu huu, ambapo kwenye michezo mitano iliyopita nimefanikiwa kufunga bao moja na kuasisti mara tano, kwangu nimekuwa nikisema mara zote kuwa natamani kufanya vizuri kwenye kila mchezo kwa ajili ya mafanikio ya Simba.

“Kiwango nilichofanikiwa kukionyesha kwenye michezo iliyopita na ushindani wa namba uliopo kwenye kikosi vimezidi kunipa ari ya kutaka kufanya vizuri zaidi, hivyo naamini nitakuwa moto zaidi kwenye michezo ijayo baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa kumalizika,” alisema kiungo huyo raia wa Msumbiji.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger