10/28/2020

"Kuanzia Leo Usiku Tutapokea Matokeo" - Mkurugenzi NEC

 


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera amesema kuanzia leo usiku Jumatano Oktoba 28, 2020 tume hiyo itaanza kupokea matokeo ya kura za urais kutoka kwenye majimbo.

Dkt. Mahera ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Mwananchi Digital kuhusu maandalizi ya kupokea, kujumlisha na kutangaza matokeo ya urais shughuli inayofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).


“Tutaanza kupokea matokeo kuanzia leo na kuendelea kwa hiyo kesho tutakuwa tuko serious kupokea matokeo kutoka maeneo mbalimbali na kuyatangaza ila matokeo ya udiwani yatatangazwa kwenye kata” Mahera


“Matokeo ya Ubunge yatakuwa yanapokelewa na kutangazwa kwenye jimbo halafu wanatutumia sisi hapa(JNICC) tunayajumlisha na kuyatangaza tena kwamba jimbo fulani tayari matokeo yake yameshatangazwa kwa nafasi ya rais” Mahera

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger