Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Lulu Diva Kupokonywa Gari la Kifahari

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREUBUYU wa mtoto uliodakwa na Risasi Mchanganyiko unadai kuwa, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anataka kupokonywa lile gari la kifahari aina ya Jeep, alilozawadiwa na mpenzi wake anayetajwa kwa jina la Joh.


Chanzo chetu makini sana ambacho kiko karibu na msanii huyo, kimesema kuwa, Joh alimzawadia gari hilo walipokuwa kwenye mapenzi na alimpa kama zawadi, tena alimwambia ni lake lote na hata kadi ilikuwa na jina lake.


“Unajua Lulu alipewa lile gari jipya kabisa na Joh na mpaka makaratasi alikuwa akiyafungua mwenyewe, na alimpa kwa sababu Lulu alikuwa akitamani sana kuendesha gari kubwa, hivyo alimfanyia kama surprise lakini kwa sasa jamaa amembadilikia ghafla,” kilisema chanzo.

Kikiendelea kuvujisha habari, chanzo hicho kilisema kuwa, Joh kwa sasa amekuwa akikinukisha mara kwa mara, akiita arejeshewe gari lake kwani yeye na Lulu uhusiano ulishavunjika siku nyingi.


“Yaani Joh akiamua kwenda na kundi lake kutaka gari lake, panakuwa hapatoshi na nia kubwa anataka kama aendelee kuwa na hilo gari, waendelee na uhusiano wa kimapenzi, kitu ambacho hakiwezekani tena kwa Lulu,” alisema mpashaji huyo.


Mtoa habari huyo anaweka wazi kuwa, Lulu amelifanyia marekebisho makubwa sana gari hilo kuanzia kubadilisha rangi na kila kitu, ndiyo maana inakuwa ngumu kulirejesha, ilhali kadi pia inasoma jina lake.

Gazeti hili baada ya kupata ubuyu huo, lilimvutia waya Lulu ambapo alikiri kupata usumbufu wa gari hilo kutoka kwa mpenzi wake wa zamani, lakini akasema aachwe atamalizana naye.


“Ni kweli tuko kwenye shida na mpenzi wangu wa zamani aliyenipa gari, lakini ukweli anaujua, nafikiri nitamalizana naye mwenyewe tu maana hilo gari limenigharimu sana,” alisema Lulu.


STORI IMELDA MTEMA, RISASI

Post a Comment

0 Comments