Lyyn Ampakulia Minyama Kiba!

 


Sexy lady wa Bongo Fleva, Irene Louis ‘Lyyn’ amempakulia minyama kama yote mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.


Katika mahojiano maalum na Gazeti la Ijumaa, Lyyn anasema;“Uhusiano wetu upo vizuri, tumeshawahi kukaa wote, tukaongea na kubadilishana mawili matatu.

 

Kiukweli amenipa ushauri kwamba wewe unatakiwa uwe hivi na hivi. Kwa hiyo madini aliyonipa ndiyo yanayonifanya niwe hapa nilipo na mengine ninayafanyia kazi.

 

Ijumaa: Kuna maneno yalisemwa kwamba baada ya kuachana na Diamond aliyekuwa mpenzi wako, sasa unataka uhamishie majeshi kwa King Kiba, kwa kujifanya unaomba kolabo, lakini kwa bahati mbaya hakukubalia, hili limekaaje?

 

Lyyn: Kiukweli sijawahi kwenda kwa Ali (Kiba) kuomba kolabo, mimi nilimjua Ali (Kiba) kwa sababu ya Tommy (msanii wa Kiba kwenye Kings Music), halafu kitu kingine mimi sijahama WCB (Lebo ya Wasafi Classic Baby) wala kwa Mondi, mimi ni msanii hivyo sitakiwi kuwa na matabaka, ninashirikiana na kila mmoja.

 

Ijumaa: Ukipewa nafasi ya kumzungumzia King Kiba kwa kifupi utakuwa na yapi ya kusema?

Lyyn: Ni mstaarabu, na mcheshi sana, ukikaa naye huboreki.

Ni mtu ambaye anapenda kila mtu afanikiwe.Lyyn aliwahi kukiri kuchumbiwa na Mondi kabla ya kuachana na kuonekana ana ukaribu na Kiba, jambo ambalo liliibua madai kwamba, huwenda anataka kuwachanganya kimapenzi.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE