Maalim Seif aahidi kulipa fidia kwa Wazanzibar ambao ardhi zao ziliathiriwa na gesi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mgombea Urais Zanzibar  kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Hamad, amesema kama wananchi watampa ridhaa ya kuongoza atahakikisha analipa fidia ambayo inatosha kwa Wazanzibar  ambao ardhi zao ziliathiriwa na gesi.

Seif ameyasema hayo leo Oktoba mosi, wakati akifanya kampeni zake Pemba ambapo amesema kuwa Zanzibar imebarikiwa mafuta na gesi asilia na kuahidi kuwa atahakikisha anaweka sera nzuri ili kusaidia kukuza uchumi.


''Zanzibar tuna mafuta na gesi asilia,tuna sera ya mafuta na gesi na wale wote ambao ardhi zao zimechukuliwa au kuathiriwa na gesi lazima walipwe fidia ambayo inatosha kabisa"amesema Maalim Seif.


Mgombea huyo ameongeza kuwa atahakikisha anawatengenezea wazanzibar mamlaka kamili ya nchi yao na pia kujenga uchumi ambao utaleta huduma nzuri za kijamii.


"Ahadi ya kwanza ni kuwatengenezea wazanzibar mamlaka kamili ya nchi yao,Tutajenga uchumi maisha ya raha na furaha,huduma nzuri za kijamii ikiwemo afya,elimu,usafiri na usafirishaji"amesema Maalim Seif


Aidha amesema kuwa atahakikisha haki moja kubwa anaitimiza ambayo ipo katika katiba ya kila mtu kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa. 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad