Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Maalim Seif adaiwa kukamatwa Zanzibar, polisi wasema hawana taarifa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Unguja. Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamad amedaiwa kukamatwa leo Jumanne Oktoba 27, 2020 kisiwani Zanzibar.


Hata hivyo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji amesema hajapokea taarifa za Maalim Seif kukamatwa na kuahidi kuzifuatilia.


Akizungumza na Mwananchi Digital, katibu wa itikadi na uenezi na mawasiliano kwa umma wa chama hicho, Salim Bimani amesema Maalim Seif amekamatwa saa 2:05 asubuhi katika kituo cha kupigia kura cha Garagara, amepelekwa makao makuu ya polisi eneo la Ziwani kwa mahojiano.


Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho alikwenda katika kituo hicho kupiga kura

Endelea kufuatilia Mwananchi Digital kwa taarifa zaidi

Post a Comment

0 Comments