Manara Sio Mtu Mzuri Aibuka na Mpya ya Kuwakera Watu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



SIMBA imekuja na kauli mbiu mpya kuelekea mechi ya watani wa jadi, itayopigwa Oktoba 18, mwaka huu kutokana na matokeo yatakayopatikana ambayo ni ‘Zin Zala Day’.


Simba ambayo imetoka kupata ushindi mnono katika mechi zake mbili zilizopita nyumbani, itacheza na JKT Tanzania keshokutwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.


Wanamsimbazi hao wanajiamini kutokana na kikosi chao na matokeo ya mwisho dhidi ya watani wao Yanga kwa kuwafunga mabao 4-1, Julai mwaka huu kwenye Dimba la Mkapa, jijini Dar es Salaam.



 

Tambo za kuelekea mchezo huo tayari zimeanza kila kona, huku Simba ikionekana kutamani zaidi siku hiyo ifike wakiamini wataendeleza ubabe.


Kwa mujibu wa  Mkuu wa Idara ya Habari Simba, Haji Manara, watatumia mchezo na JKT Tanzania kama maandalizi ya kuikabili Yanga kwa sababu kutakuwa na mapumziko ya kupisha ratiba ya timu ya Taifa, Taifa Stars.


Alisema mchezo wao wa Oktoba 11, waliotakiwa kucheza baada ya JKT Tanzania, umeahirishwa, hivyo wakitoka Dodoma, kitakachofuata ni Yanga.


“Tunakwenda kucheza mechi ya mwisho kabla ya kukutana na watani wetu Yanga tarehe 18, mchezo wetu wa tarehe 11 umeahirishwa kutokana na ratiba ya mchezo wa  timu ya Taifa, Taifa Stars.


“Naamini katika kipindi hicho, mwalimu atakuwa amekamilisha program za maandalizi yake, tunajua matokeo yatakavyokuwa na mtani wetu ni ‘zin zala day’,” alisema.


Katika hatua nyingine, Manara alisema kikosi chao kinatarajia kuondoka leo, kuelekea Dodoma lakini kitalala Morogoro kufanya sherehe za ubingwa na mashabiki  wao, walioomba kufanya hivyo.


“Mashabiki waliomba timu ipitie Morogoro ili walione kombe la ubingwa, Ijumaa tutakuwa na kombe hilo Moro kila shabiki atapata fursa ya kuliona na Jumamosi tutakwenda Dodoma,” alisema.


Manara alieleza kikosi chao kipo vizuri, wakiwa hawana majeruhi zaidi ya Gerson Fraga na John Bocco ambaye anaendelea vizuri na program ya mwalimu na huenda wiki ijayo akarejea uwanjani.


Manara aliwataka mashabiki wote wa Simba wa Jiji la Dodoma na wale wa mikoa ya jirani, kujitokeza uwanjani Jumapili kuipa sapoti timu yao.


“Tunaomba mashabiki wote wa Simba wajitokeze uwanjani, hata wale wa Yanga pia tunawaruhusu waje na jezi zao kutuzomea, hakuna atakayepigwa wala kufinywa, Simba ni wastaarabu na wakizomewa waona raha na  kuwaongezea mzuka wachezaji,” alisema Manara.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad