10/08/2020

Marioo Amuacha Mondi Aruke na Mimi Mars!DAR: Staa wa Bongo Fleva anayefanya poa kwa sasa, Omari Mwanga ‘Marioo’, amekubali kumuachia kinara wa muziki nchini Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aruke na mtoto wa kike kwenye Bongo Fleva, Mariane Mdee ‘Mimi Mars’.

Hayo yamekuja, baada ya hivi karibuni kuibuka ukaribu kati ya Diamond au Mondi na sexy lady huyo kutoka Arachuga, ambaye mwanzo ilisemekana ana uhusiano wa kimapenzi na Marioo.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Marioo amesema kuwa, hata ikitokea Mondi akamchukua mwanamke wake, yeye hana shida, anamuachia tu kwa sababu anastahili.

“Mara nyingi nimekuwa nikiulizwa kuhusu uhusiano wangu na nimekuwa nikijibu vizuri kabisa, siwezi kujinyonga kama jinsi watu walivyofikiria, bali ilikuwa ni njia ya kutambulisha ngoma yangu mpya.

“Kuhusu ishu ya Mimi Mars, mimi niko sawa kabisa, nina uhusiano mzuri na Diamond Platnumz, ni kaka yangu, ni mtu mkubwa sana, watu wanamtazama kwa jicho lake.

“Kwa jinsi ninavyomheshimu Diamond, kama itatokea nikawa na mwanamke mzuri, halafu yeye akamtaka, siwezi kumchukia kwa sababu anastahili na nitaendelea kumshukuru tu,” amesema Marioo ambaye kwa sasa anakimbiza na ngoma yake ya Asante.

Stori: Happyness Masunga, Ijumaa


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger