Maskini..Mbowe apewa ONYO na Polisi Kilimanjaro

 


Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limetoa onyo kwa mgombea Ubunge jimbo la Hai kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, baada ya mgombea huyo kutaka kufanya mkutano siku ya jana mahali ambapo hakutakiwa kuwepo.


Akizungumza hii leo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Emmanuel Lukula, amesema kitendo hicho si sahihi na kuwataka baadhi ya wagombea kuheshimu sheria, Kanuni, taratibu zilizowekwa na Tume ya uchaguzi.


''Mgombea wa CHADEMA wilaya ya Hai alitaka kufanya mkutano mahali ambapo hakupaswa kuwa pale  lakini Polisi tulimuelimisha lakini pia tukamtaka asifanye hivyo,yeye kwenye eneo hilo amepangiwa kufanya mkutano tarehe Oktoba 14'' amesema Kamanda Lukula


''Kama jana angefanya mkutano lakini kijiji jirani na nadhani ndio njia ya kupita walikuwepo wenzao wa Chama cha Mapinduzi watu wana mihemko tofauti tofauti  mnaweza mkafanyiana fujo polisi tukaingia kwenye kazi nyingine'' ameongeza Kamanda Lukula


Aidha ametoa wito kwa wagombea kwa ngazi yoyote ile kuheshimu miongozo ya Tume ya uchaguzi ambapo amesema inarahisisha kazi ya ulinzi na usalama.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE