Mbatia apinga kufungiwa, kuendelea na kampeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



JAMES Mbatia, Mgombea Ubunge wa Vunjo Mkoa wa Kilimanjaro kupitia NCCR-Mageuzi, ameupinga uamuzi uliotolewa na Kamati ya Maadili Jimbo hilo wa kumfungia kwa siku saba kutokufanya kampeni kuanzia leo Jumamosi tarehe 17 hadi 23 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).


Uamuzi huo ulitolewa jana Ijumaa na kikao hicho, baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwasilisha malalamiko kwamba, Mbatia anatumia vipeperushi ambavyo havijasajiliwa na msimamizi wa uchaguzi.



 

Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-Mageuzi, Edward Simbeye akizungumza na MwanaHALISI ONLINE amesema, “uamuzi huo ni batili, kikao kilichofanyika ni batili na tunaendelea na kampeni kama kawaida.”


Simbeye aliyeko jimboni kwa Mbatia amesema, vipeperushi vinavyozungumzwa vinaelezea mambo aliyoyafanya Mbatia kwa kipindi cha miaka mitano (2015-2020).


Amesema, kwa mujibu wa Maadili ya Uchaguzi kipengele cha 5:4 kinazungumzia, kama kuna maadili yamekiukwa, “kiwasilishe kwa msimamizi kwa njia ya maandishi, lakini CCM haijafanya hivyo, tuliomba kupewa hayo malalamiko yao kwa maandishi, hatukupewa.”



Edward Sembeye, Mkuu wa Mawasiliano ya Umma NCCR-Mageuzi

Simbeye amesema, baada ya Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi kupewa malalamiko hayo, “aliyajibu lakini cha kushangaza, katika kikao cha jana utetezi wake aliouwasilisha kwa maandishi, haukusomwa, sasa unawezaje kuamua bila kusikiliza utetezi wa anayelalamikiwa.”


Pia, amesema, kikao kilichokaa jana, kilihusisha majimbo mawili jambo ambalo ni kinyume na taratibu za uchaguzi “yaani mgombea wetu, amehukumiwa na vikao viwili vya majimbo badala ya kimoja. Ndiyo maana tunasema ni batili na sisi tutaendelea na kampeni kama kawaida kesho.”



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad