10/12/2020

Mboto Agoma Carlinhos Kuitwa Mkata UmemeALIYEKUWA mjumbe wa kamati ya hamasa ya Yanga, Mboto Haji, amesema Carlos Fernandes de Carmo ‘Carlinhos’ ndani ya kikosi cha timu hiyo ni mng’oa nguzo na siyo mkata umeme.


Mchekeshaji huyo aliyazungumza hayo baada ya mchezo wa kirafi ki dhidi ya Mwadui FC, uliopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi jijini Dar ambapo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.


Katika mtange huo, mshambuliaji wa klabu hiyo, Michael Sarpong, ndiye aliyeibuka kuwa mchezaji bora ambapo alipachika bao pekee la ushindi dakika ya 81 ya mchezo baada ya kupokea pasi kutoka kwa Carlos Carlinhos.


Akizungumza na Championi Jumatatu, Mboto alisema kuwa kwa sasa timu hiyo ina wachezaji wazuri kutokana na usajili uliofanyika jambo ambalo linapelekea wachezaji kucheza ‘pira biriani’.


“Yanga tuna wachezaji wazuri baada ya kufanya usajili ambao una tija kutokana na aina ya wachezaji waliopo ukimwangalia Carlinhos akiingia uwanjani ni mng’oa nguzo na siyo mkata umeme kama wanavyomuita,” alisema Mboto.


LEEN ESSAU, Dar es Salaam

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger