Mdahalo kati ya Biden na Trump kufanyika Ijumaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mdahalo wa mwisho kati ya rais Donald Trump na mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden utafanyika siku ya Ijumaa na watayarishaji wameweka masharti maalum kuzuwia hali ya wagombea hao kulumbana bila mpangilio kama ilivyotokea mara ya kwanza. 

Kutakuwa na kitufe cha kufunga kipaza sauti cha kila mgombea ili kuzuwia hali ya kuingiliana wakati wa kuzungumza, wamesema watayarishaji leo, wakitaka kuzuwia hali iliyojitokeza katika mdahalo wa kwanza. 


Meneja wa kampeni ya Trump, Bill Stepien amesema kwamba rais huyo yuko tayari kufanya mdahalo huo na Joe Biden bila kujali mabadiliko ya dakika za mwisho ya sheria. 


Zaidi ya Wamarekani milioni 30 wamekwisha piga kura zao, wakipunguza uwezekano wa Trump kubadilisha hali ya mwelekeo katika nchi hiyo ambayo inaonesha kuwa yuko nyuma katika maoni ya wapiga kura kitaifa na katika majimbo.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad