Membe: Hata Mninyonge, Wabunge 32 Siwataji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MGOMBEA urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe, amesema  kabla hajafukuzwa na chama chake cha awali cha CCM, alikuwa anao mpango wa kukipindua chama hicho kiuongozi kwa kushirikiana na watu wengine sita na alikuwa na jumla ya wabunge 78.


 


Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba, 19, 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo pia ameeleza mustakabali wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, 28, mwaka huu, kwa kuuaminisha umma wa Watanzania kuwa yeye ndiye mgombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo.


 


“Mimi nilikuwa CCM nikataka kukabiliana na rais aliyepo madarakani peke yangu kumuondoa, lakini washukuru walinifukuza, tulijianda na wana-CCM wenzangu, achilia mbali tulikuwa watu sita tuliokuwa tayari kuiondoa serikali madarakani, mimi nilikuwa na wabunge 78, kwa bahati mbaya 46 wamefyekwa lakini wako CCM 32 wamebaki.  Hata mkininyonga siwezi kuwataja kwa sababu watatumbuliwa tu,” amesimulia Membe.


 


Aidha, Membe ameongeza kuwa, “Kuungana kwa vyama vya upinzani ni lazima chama tawala kipasuke ili kundi la pili lije upande wa pili ili kusaidia chama tawala kuangushwa.   CCM mwisho wake umefika na tunawaondoa madarakani Oktoba 28.”


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad