Moto Wote Wadhibitiwa Mlima Kilimanjaro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




SHIRIKA  la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limesema kuwa ukaguzi wa anga uliofanywa jana asubuhi, Oktoba 16, 2020, katika Mlima Kilimanjaro umebaini kuwa moto wote umedhibitiwa lakini vikosi vya askari vimetawanywa kwa ajili ya tahadhari.


 


Moto huo uliozuka Oktoba 11 mwaka huu umeathiri eneo la kilomita za mraba 95.5 ambazo ni sawa na 5% ya eneo lote la hifadhi lenye kilomita za mraba 1,700.


 


TANAPA imesema kuwa udhibiti wa moto huo umetokana na kazi kubwa inayoendelea kufanywa na askari, wananchi na Jeshi la Zimamoto. Licha ya moto huo, shughuli za utalii katika Mlima Kilimanjaro zinaendelea kama kawaida.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad