10/09/2020

Mourinho Awataja Walioimaliza Man UnitedKOCHA wa Tottenham, Jose Mourinho amesema kuwa aliwatuma mabeki wake, Serge Aurier na Sergio Reguilon kuhakikisha wanadili na Marcus Rashford na Mason Greenwood, ndiyo maana wakafanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1.


Wikiendi iliyopita, Spurs ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Old Trafford, iliibuka na ushindi huo wa mabao 6-1 dhidi ya Man United.

Mourinho alisema, aliwaelekeza mabeki wake hao nini cha kufanya huku akiwa amewalenga Rashford na Greenwood alioamini ndiyo hatari ndani ya Man United.


“Niliwaambia wachezaji wangu zaidi ya mara 1000 kuwa wanatakiwa kushinda pale Old Trafford. Na niliwapa maelekezo mabeki wangu nini cha kufanya na wadili na nani.

“Aurier na Reguilon wakishirikiana na wenzao niliwaeleza wadili zaidi na Rashford na Greenwood na hilo walifanikiwa.”


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger