10/11/2020

Msuva: Tunaanza na Burundi, Tunisia Wajiandae
NYOTA wa Kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa kwenye Klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco, Simon Msuva, amewajaza matumaini Watanzania akisema kwamba leo watapata matokeo mazuri kwenye mchezo wa kirafi ki wa kimataifa dhidi ya Burundi.


 


Leo Jumapili, Taifa Stars ikiwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar, itachezadhidi ya Burundi kuanzia saa 10:00 jioni ambapo Msuva anasema ushindi utawafanya kuongeza matumaini ya kufanya vizuri kwenye michezo ya kutafuta tiketi ya kushiriki AFCON 2022 dhidi ya Tunisia.
Akizungumza na Spoti Xtra, Msuva alisema: “Tuna kibarua kizito cha kuhakikisha tunapata matokeo mazuri dhidi ya Burundi ili kuongeza matumaini kuelekea michezo ya kufuzu AFCON dhidi ya Tunisia.
“Tunajua mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha Burundi ambao tayari tumewahi kucheza nao mara kadhaa ikiwemo michezo miwili ya kufuzu hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia na kila mmoja aliona upinzani tuliokutana nao. Tunaanza nao, kisha Tunisia watatusubiri.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger