Mtoto Ampa Heshima Kim Nana DAR : Muuza nyago maarufu (video vixen) Bongo, Lillian Kessy ‘Kim Nana’, amesema kuwa, mwanaye Sky ndiye kila kitu kwenye maisha maana bila yeye asikuwa hapo alipo.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Kim Nana ambaye amejifungua miezi michache iliyopita amesema kuwa, mwanaye huyo ni mtu ambaye amempa mabadiliko makubwa kwenye maisha yake na kwa sasa watu wanamuheshimu tofauti na kipindi cha nyuma.

“Huyu mtoto ameleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yangu, Kim wa mwaka mmoja uliopita ni tofauti na Mama Sky au Mama Keeza wa sasa. Kwa kweli amenipa heshima kubwa, ninampenda sana mwanangu,” anasema Kim Nana.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE