Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Nigeria yakanusha kuhusika na kukamatwa kwa waandamanaji Misri

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURESerikali ya Nigeria imekanusha kujihusisha na kukamatwa kwa waandamanaji wa End SARS katika mji wa Cairo nchini Misri.

Msemaji wa Tume ya wanaoishi Ughaibuni ya Nigeria, Abike Dabiri-Erewa, amesema mamlaka ya Misri ilianza kuwakamata wanaoandamana.


Aliongeza kuwa raia wa Nigeria hawakukamatwa katika ubalozi wao lakini ubalozi huo uliwasiliana na mamlaka ya Misri ichukue hatua.


Maandamano ya #EndSARS, ambayo yanadai kumalizika kwa unyama unaotekelezwa na polisi umeenea katika maeneo mbalimbali duniani huku walio ughaibuni wakionesha kuwaunga mkono wenzao wa nyumbani.


Serikali ya Nigeria ilivunja kikosi maalum cha kukabiliana na wizi wa mabavu kinachochukiwa na raia lakini bado wanataka mabadiliko kamili katika kikosi hicho.Post a Comment

0 Comments