10/21/2020

Nyumbani kwa Jackline Mengi, Mafuriko Yalivyoharibu Vitu vya Thamani (+video)


 Jacqueline Mengi ni miongoni mwa baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam ambao nyumba zao zilikumbwa na adha ya mafuriko kwenye mvua zilizonyesha Jumanne na Alhamis wiki iliyopita.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jacqueline ametuonesha namna nyumba yake ilivyoharibiwa mara baada ya maji kuingia ndani pia vitu vyake vya thamani vikiharibika vibaya.


Kubwa ambalo amesema lilimtoa machozi mbele ya watoto wake mapacha ni kuharibika kwa vitu ambavyo ni zawadi zilizoachwa na marehemu Mzee Mengi ambavyo vilibaki kama kumbukumbu kwake na kwa watoto wake.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger