10/15/2020

Pogba aitamani Barcelona, Ozil akataa mshahara mnono SaudiaKiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 27, anataka kujiunga na Barcelona kwa uhamisho huru dirisha lilajo la usajili la majira ya joto. (Mundo Deportivo, via Sun)Kiungo wa Arsenal, Mjerumani Mesut Ozil, 31, mapema mwezi huu alikataa ofa ya mshahara wa £200,000 kwa wiki kuondoka kwa washika bunduki hao na kutua ligi ya Saudi Arabia (SPL). (Fabrizio Romano, via Express)


Mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger, 27, amesema anataka kurejesha nafasi yake ndani ya kikosi cha Chelsea baada ya uhamisho wake kukwama katika dirisha la usajili lililopita.. (Athletic – subscription required)


Mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 32, hana mpango wa kuhamia Italia licha ya kusakwa na klabu ya Inter Milan ya ligi ya Serie A. (Fabrizio Romano, via Sports Illustrated)Sergio Aguero


Chelsea wanajiandaa kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na kiungo wake kutoka Italia, Jorginho, ambaye alihusishwa na mipango ya kuhamia Arsenal wakati wa dirisha la usajili lililopita. (AreaNapoli, via Express)


Meneja wa zamani wa Juventus Max Allegri anaweza kuwania nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer , kama Manchester United itamtimua kocha wake huyo. (Express)


Mshambuliaji wa Liverpool na Switzerland Xherdan Shaqiri, 29, amesema aliamua kubaki kwenye klabu yake wakati wa usajili wa majira ya joto, licha ya kuhusishwa kutaka kuondoka kwa mabingwa hao wa ligi kuu ya Engalnd. (Mail)Xhedan Shaqiri


Manchester United haikuwasilisha ofa yoyote kwa ajili ya mshambuliaji wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman, 24, wakati wa dirisha la usajili, anasema mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo ya Ujerumani Hasan Salihamidzic. (Bild, via Mail)


West Brom imekubaliana ada ya uhamisho ya karibu £15m na klabu ya Huddersfield kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji wa Kiingereza Karlan Grant, 23. (Sky Sports)


Juventus imeungana na Manchester City katika mbio za kumuania mlinzi wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28. (Sportmediaset, via Manchester Evening News)


Liverpool wako tayari kumuachia kwa mkopo Harry Wilson , lakini ilikataa ofa ya Swansea City kwa ajili ya winga huyo mwenye umri wa miaka 23. (Athletic, via Wales Online)David Alaba


Wilson ni mmoja wa wachezaji watano ambao wekundu hao wa Anfield wanataka kuwauza kwa mkopo. (Express)


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger