Polepole atoa ujumbe katika majimbo watakayoshinda

 


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, (CCM),Humphrey Polepole amewataka wagombea watakaoshindwa katika majimbo yao kuandaa utaratibu mwingine wa kujitafutia kipato ikiwemo kujikita katika kilimo kwani si lazima kuwa Mbunge.Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, (CCM),Humphrey Polepole


Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi ndogo ya chama Lumumba, jijini Dar es salaam, Polepole ameitaja Kigoma mjini kuwa miongoni wa jimbo watayoshinda kwenye uchaguzi huu.


“Ni vizuri wale katika majimbo ambayo tutashinda kwa kishindo watu waanze kujiandaa kuweka utaratibu mwingine ziko biashara ,kilimo na vitu kama hivyo si lazima ukawa mbunge” alisema Polepole


Akiwa anaelezea juu ya ajali aliyoipata  Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, Polepole amesema sera nzuri za chama chake ndio zilizochangia kunusuru uhai wa kiongozi huyo.


“Leo hii yule bwana anaweza kuona mkewe na familia kwasababu ya sera nzuri za Chama cha Mapinduzi na sisi kama chama tunamtakia kupona haraka aimarike mapema” alisema Polepole


Aidha Polepole amesema kuwa mgombea wa urais wa chama cha CCM Dkt.John Magufuli atafanya kampeni zake jijini Dar es salaam kesho kuanzia saa mbili asubuhi katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE