Polisi Waeleza Sababu Tatu Kutumia Mabomu ya Machozi Zanzibar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


By Haji Mtumwa, Mwananchi hmtumwa@mwananchi.co.tz

Unguja. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi  kisiwani Zanzibar limesema limelazimika kutumia mabomu ya machozi katika baadhi ya maeneo kutokana na uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani.


Limesema waliokamatwa ni waliochoma matairi na kuyaweka katikati ya barabara na waliokwenda katika vituo vya kupigia kura wakati leo wanaoruhusiwa kupiga kura ni makundi maalum wakiwemo askari wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na kuyashambulia kwa mawe magari ya polisi.


Hayo yameelezwa leo Jumanne Oktoba 27, 2020 na Kamanda Polisi wa Mkoa huo, Awadh Juma Haji wakati akizungumza na Mwananchi Digital.


Amesema mbali ya matumizi ya mabomu hayo, wanawashikilia baadhi ya vijana waliodai kuhusika katika matukio hayo.


Amebainisha kuwa vijana hao wanatuhumiwa  kuchoma moto matairi ya magari na kuyaweka katikati ya barabara na maeneo mbalimbali kinyume na sheria, kuyashambulia kwa mawe  magari ya askari polisi waliokuwa katika doria  huku wakijua kuwa kazi ya polisi ni kusimamia amani na utulivu.


Amesema walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliofika katika vituo vya kupigia kura kwa lengo la kupigakura wakati wakijua leo wanaohusika katika shughuli hiyo ni makundi maalum.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad