10/22/2020

Polisi Watu Rais 12 NigeriaVIKOSI vya usalama nchini Nigeria vimeyavyatulia risasi makundi mawili ya waandamanaji na kuua watu 12 waliokuwa wakishinikiza polisi kuacha kutumia matumizi ya nguvu dhidi ya raia katika jiji la Lagos.

Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu duniani — Amnesty International — tangu kuanza kwa maandamano hayo wiki mbili zilizopita, inakadiriwa zaidi ya watu ya 50 wamepoteza maisha.

Pamoja na kutokea kwa vifo hivyo bado makundi makubwa ya waandaamanaji wameendelea kuingia mitaani na kuanza kuchoma matairi moto, huku wakiimba wimbo wa taifa hilo.

Watu maarufu nchini humo akiwemo msanii Davido wameungana na waandamanaji waopinga vikali vitendo hiyo, akitumia mtandao wa Instagram kumwonyesha Rais Mahamoud Buhari na kusema “tulikosea kukuchagua haya ndio malipo yake.”


Watu maarufu duniani akiwemo Beyonce, Kanye West, Rihhana na Hillary Clinton wamepaza sauti zao kuhusu maandamano hayo

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger