10/20/2020

Raia wa kigeni wakamatwa wakiingiza dawa za kulevya EthiopiaPolisi nchini Ethiopia wamewakamata washukiwa 14 kwa kujaribu kuingiza dawa za kulenya aina ya kokeini kupitia uwanja mkubwa wa ndege mjini Addis Ababa.

Polisi nchini humo wamesema washukiwa 13 raia wa Nigeria na mmoja wa Brazil wamepatikana na kilo 14 za dawa za kulevya aina ya kokeini katika mabegi yao, nguo za ndani na baadhi zilikuwa wamezimeza.


Washukiwa hao walikuwa wamewasili Sao Paulo, Brazil, Jumatatu.


Walikamatwa na kuzuiliwa uwanja wa ndege, kwa mujibu wa kamanda anayeshughulikia oparesheni ya dawa za kulevya Mengisteab Beyene.


Polisi waliongeza kusema kuwa Ethiopia imenasa kilo 39 za dawa za kulevya aina ya kokeini na kilo 36 za bangi kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger