Rais Magufuli Atoa Ya Moyoni Kuhusu Dr Wilbrod Slaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,John Magufuli amefichua siri jinsi alivyomfahamu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na Mbunge wa Jimbo la Karatu  Balozi Dkt.Willibroad  Slaa kwa jinsi alivyokuwa tofauti na wapinzani wengine.


Balozi Dkt.Slaa alihama Chadema wakati  vuguvugu la uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa Chama hicho kikiungana  na vyama vilivyokuwa vikiunda UKAWA kumpitisha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kuwa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano .


Mbali na Chadema vyama vingine vilikuwa ni Chama cha Wananchi CUF,NCCR Mageuzi na NLD.


Akizungumza hayo leo, jimboni  karatu mkoani Arusha kwaajili ya kuomba kura kwa wananchi,Magufuli amesema Balozi Dkt.Slaa alikuwa ni tofauti na wapinzani wengi  kwa jinsi  alivyokuwa mtu makini,mwenye kujenga hoja na alikuwa mwakilishi mzuri wa wananchi wa jimboni kwake.


Magufuli amesema kwake yeye  kama kuna mtu mmoja kwenye vyama vya upinzani ambaye anaweza akasema huyu ni kweli alikuwa Mpinzani kwaajili ya watu ,Mzalendo wa kweli na  Muadilifu ni Balozi,Dkt Slaa.


Balozi Dkt.Slaa alikuwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja ,kuchagua maneno ya kuzungumza,muadilifu na mzalendo wa kweli .


Amesema kwa kutambua uwezo na kuamini kuwa  kuna mpinzani mmoja kati ya wapinzani wote waliopo Tanzania wa kweli aliamua kumteua Balozi Dkt.Slaa kuwa balozi wa nchi Tisa.


 “Wakati alipotaka kuja kuomba ubunge huku (karatu)aliomba nafasi hiyo kupitia Chama cha Mapinduzi kwasababu yeye alikuwa mwanaccm,Chama cha mapinduzi hapa karatu wakamfanyizia figisu hawakulirudisha jina lake ndipo akaamua kwenda mageuzi,”amesema na kuongeza


“Balozi Dkt.Slaa baada ya kukaa upinzani na kuona ubabaishaji kwenye Chama hicho aliamua kujitoa katika Chama hicho,”amesema


Amesema hata alipokuwa bungeni alivyochaguliwa alikuwa mtu makini,mwenye kujenga hoja,anawakilisha mawazo ya wananchi waliokuwa chini,hali hiyo iliwafanya hata watu waliokuwa CCM kumpenda katika kipindi chake.


 “Inawezekana namna alivyo ilitokana na kazi yake aliyofanya ya Upadri na kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania…kwangu Mimi kama kuna mtu mmoja kwenye vyama vya upinzani ambaye anaweza akasema huyu ni kweli alikuwa kwaajili ya watu basi ni Balozi Dkt.Slaa,”amesema na kuongeza


 “Dkt.Slaa alikuwa mstaarabu tofauti na wapinzani tunaowaona leo ambao  wakiingia bungeni hawajengi hoja,Mkitangaza bajeti kwaajili ya wananchi wa karatu na maeneo mengine wao hawawasapoti,mkijadili bajeti kwaajili ya maendeleo ya wananchi wao wanatoka nje siku nyingine wanaweka plasta midomoni,”amesema


Amesema katika maisha yake yote alivyokuwa Mbunge hakuwahi kumuona Balozi Dkt.Slaa akiweka plasta katika mdomo akiwa bungeni.


“…Ndio maana nasema kwa ukweli kutokana na uwezo mkubwa wa mwanamapinduzi wa Dkt.Slaa na kutokana na upendo alionao kwa wananchi bila kubagua vyama niliamua kumteua kuwa balozi kuwakilisha Tanzania katika nchi tisa.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad