10/16/2020

Raja Casablanca Yamtaka Prince DubeMTANDAO maarufu wa Soccer24 umeripoti kwamba, vigogo wa Morocco, Raja Casablanca wameweka ofa ya dola za Kimarekani milioni moja (US $1m) ili kumnasa Prince Dube kutoka Azam FC.

Inaelezwa kuwa, Raja wamevutiwa na uwezo wa raia huyo wa Zimbabwe ambaye mpaka sasa anaongoza kwa ufungaji wa mabao katika Ligi Kuu Tanzania bara akiwa na mabao matano mbele ya Medie Kagere, lakini Azam imeonekana kutokukubali ofa hiyo.

Mtandao wa Soccer24 umemnukuu mtu ambaye jina lake halijatajwa akisema, ni kweli Raja imevutiwa na mchezaji huyo na kumekuwa na kiasi cha pesa kikitajwa lakini mchongo huo itakuwa ngumu kutiki kwa sababu hawatakuwa tayari kumwachia pengine hadi mwisho wa msimu huu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger