ROMA Mkatoliki Awalipua Madaktari Wanaotengeneza Madhingira ili Wajawazito Wajifungue Kwa Operation Badala ya Njia ya Kawaida

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


 Kutoka kwenye ukurasa wa msanii @roma_zimbabwe ameandika maneno haya:

"Hospitali Nyingi Tunapowapelekaga Wake Zetu Na Wachumba Zetu Na Dada Na Mama Na Shangazi Na Rafiki Zetu  Wa Kike ili Wakajifungue.

Mara Nyingi Utakuta Madaktari Mnatengeneza Mazingira ili Tu Wenza Wetu Hawa Wajifungue Kwa Njia Ya Operation!! Kwa Maana Gharama Yake Ni Kubwa Kuliko Njia Ya Kawaida!!

Hata Kama Mtu Anauwezo Wa Kupush Kwa Njia Ya Kawaida, Mtasema Tu Njia Yake Ya Uzazi Ni Ndogo, Hii Kauli Imekuwa Kawaida Kwa Wajawazito Wengi Sikuhizi!! Mara Atawekewa Dripu La Uchungu Na Lisi-Function, Ili Mradi Tu Tu-Sign Ile Karatasi Mtu Apigwe Kisu!!

Mnawaweka Vilema,Alama Na Makovu Wachumba Zetu Kwa Maslahi Yenu Binafsi!! Inatuumiza Sana Sisi Waume Zao, Hata Na Wao, Ingawa Wanakuwa Hawana Jinsi Wala Maamuzi Kutokana Na Hofu!!

Nways Sio Hospital Zote Na Sio Madaktari Wote, ila Tunao Wengi Tu Wanaotenda Hayo Na Tunaishi Nao Na Tunashuhudia Hayo!!Narudia Tena Sio Wote,Ila Wapo Baadhi Waliokosa Weledi Katika Field Yao Hii!!

Nakubali 💯Operation Ni Nzuri Na Salama, Lakini Ifanyike Inapobidi, Isiwe Kwa Maslahi Hasa Ya Pesa,Mishahara Najua Haitoshi, Lakini Hata Sisi Tunatafuta Kwa Shida Sana, So Tusiwape Vidonda Mama Zetu!!

Nawapenda Dada Zangu Wote Na Naelewa Maumivu Yenu!! Mungu Awape Uzao Ulio Mwema Na Salama ❤️❤️ Amina Inshallah 🙏 Asalam Aleykum!!"

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad