Salah, Mane yupi atauzwa kumpisha Mbappe Liverpool

 


Liverpool kwa muda mrefu imekuwa ikihusishwa na nia yake ya kutaka kumsajili nyota wa klabu ya Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe lakini hata hivyo miamba hiyo ya soka kutoka England italazimika kumuuza mchezaji wake mmoja kati ya Mohamed Salah na Sadio Mane.

 

Mbappe mpaka sasa mkatabe wake na PSG utakifikia mwisho mwaka 2022, wakati Liverpool imeonyesha nia ya kumsajili Mfaransa huyo msimu ujao wa majira ya kiangazi.


Hata hivyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kuwa Mfaransa huyo anashauku kubwa ya kutaka kutimka msimu ujao.


Real Madrid ni moja kati ya klabu ambazo zimekuwa zikihusishwa kwa karibu na kuhitaji huduma ya nyota huyo lakini Premier League imekuwa ikipewa nafasi kubwa ya kuwezekano wa staa huyo kutua.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE