10/01/2020

Shirika la WHO Laomba Msaada wa Mabilioni kwa Ajili ya Chanjo

 


 Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) laomba msaada wa karibu dola bilioni nyingine kusaidia chanjo ya kimataifa na mpango wa matibabu dhidi ya Covid-19.

Serikali, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi zimeahidi karibu dola bilioni 1 katika mkutano huo kusaidia mpango wa chanjo na matibabu duniani.


ACT Accelerator inakusudia kutoa dozi bilioni 2 za chanjo, matibabu milioni 245 na vipimo milioni 500 ifikapo mwisho wa 2021 na hii itahitaji dola bilioni 35. Mpaka sasa zilikuwa zimepatikana dola bilioni 3.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres ametaka msaada wa dharura wa dola bilioni 15 ili kuendelea na kazi ya sasa ya mpango wa chanjo duniani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger