10/04/2020

Simba yaiadhibu JKT TanzaniaMabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara, Klabu ya Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania FC katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mshambuliaji Medie Kagere aliipatia Simba bao la kwanza kwa kichwa dakika ya tatu baada ya kumalizia mpira uliopigwa na kiungo Rally Bwalya.

Dakika tatu baadaye Chris Mugalu aliifungia Simba bao la pili kwa kichwa, baada ya kumalizia krosi iliyopigwa na Luis Miquissone

Kagere tena akatupia bao la tatu dakika ya 40 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akipokea pasi mpenyezo iliyopigwa na Clatous Chama

Dakika ya 54 Luis Miquissone alitupia bao la nne kwa shuti kali la mguu wa kushoto nje ya 18 kufuatia shuti la Kagere kuzuiwa na walinzi wa JKT Tanzania.

Mwamuzi Hance Mabena kutoka Tanga aliwaonya wachezaji Miquissone na Pascal Wawa kwa kuwaonyesha kadi ya njano kutokana mchezo usio wa kiungwana.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha alama 13 sawa na watani wao Yanga wakiizidi alama moja Azam FC ambayo usiku inacheza na Kagera Sugar

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger