10/08/2020

SUGU: CHADEMA WAKICHAGULIWA SADAKA ZITAONGEZEKA KWENYE NYUMBA ZA IBADAMgombea Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CHADEMA, Joseph Mbilinyi amewaomba Viongozi wa Dini wawaombe waumini wachague Wagombea wa Chama hicho, ili waweze kutoa sadaka kwenye nyumba za ibada


Sugu amesema maisha ni magumu na sadaka zimepungua Makanisani kwa kuwa waumini hawana fedha, hivyo kusababisha Viongozi wa Dini nao kuishi maisha magumu


Amesema, “Viongozi wa Dini sio tu mtuombee kwa Mungu ili tushinde Oktoba 28 bali pia, mtuombee kura kwa waumini wenu kwa sababu Serikali ya CHADEMA ina sera nzuri za uchumi zinazokwenda kurudisha kipato kwenye mifuko ya waumini wenu ili sadaka ziongezeke"

-

Aidha, amewataka wananchi waliojiandikisha kupiga kura wasikubali kurubuniwa na watu wanaopita majumbani kuulizia vitambulisho.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger