Tabia 10 Unazotakiwa kujifunza kutoka kwa Watu waliofanikiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 Ikiwa wewe ni mjasiriamali unayeanza au umeajiriwa sehemu fulani, kuna tabia ambazo unatakiwa kuzifahamu na kuzifanya ili uwe na mafanikio.

“Mafanikio sio zaidi ya tabia chache  rahisi zinazotekelezwa kila siku.”


Jim Rohn


Watu wengi hufikiri kuwa mafanikio ni jambo linalotokea kwa bahati tu; lakini mafanikio ni matokeo ya tabia au mikakati inayofanywa mara kwa mara.




Hivi leo kuna watu tunaowachukulia kuwa wamefanikiwa; watu hawa wana tabia fulani za msingi zinazofanana. Karibu nikufahamishe tabia 10 za watu waliofanikiwa ambazo unaweza kujifunza ili uweze kufanikiwa.


1. Wana mipango


“Tumia muda wako kutafakari ni fursa ipi uifanyie kazi na anza kuifanyia kazi kama mbwa mwitu waliopatwa na kichaa”


Neal Goldman


Watu waliofanikiwa hawafanyi kazi bila mipango madhubuti. Watu hawa hupanga mipango mbalimbali wanayotakiwa kuitekeleza; mwishoni hukagua kama mipango yao wameitekeleza jinsi ipasavyo.


Ni muhimu kujifunza tabia hii ya kujiwekea mipango na kufanya mambo kulingana na mipango husika bila kusahau kufanya tathimini mwishoni.


2. Hawaahirishi bali wanafanya


Watu waliofanikiwa hawana tabia ya kuahirisha mambo, bali huyafanya kadri wapatapo muda. Mara nyingi watu wa kawaida hujidanganya kuwa kuna muda, kesho ipo, nitafanya baadaye n.k.


Ikiwa tunataka kufanikiwa, ni lazima tufanye mambo bila visingizio wala kuahirisha.


“Tunaweza kutazama likitokea, au tukawa sehemu yake”


Elon Musk


3. Wanafanya kazi kwa bidii


Ni rahisi kufikiri kuwa watu waliofanikiwa wanalala au kukaa tu na pesa zinawajia. Watu waliofanikiwa wanajua nini maana ya kufanya kazi kwa bidii kweli.


Hakuna kitu kizuri kinachokuja kwa urahisi. Ni lazima kufanya bidii na kuwa na nidhamu ya kazi ndipo tunaweza kuona matokeo mazuri.


“Kila siku naamini ukiweka juhudi kwenye kazi matokeo yatatokea.”


Michael Jordan


4. Wanafanya wanachokipenda


“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.”


Marsha Sinetar


Je unapenda unachokifanya? Siri moja wapo ya kufanikiwa katika jambo lolote ni kufanya kile unachokipenda.


Watu wengi waliofanikiwa wanafanya kile wanachokipenda ndiyo maana wanakifanya kwa bidii na kwa ufanisi mkubwa.


Ni muhimu kujifunza tabia hii ya kufanya kile unachokipenda kutoka kwa watu waliofanikiwa ili tuweze kufikia ndoto zetu.


5. Wanaweka malengo


Hakuna mtu yeyote aliyefanikiwa bila malengo chini ya jua. Malengo ni mwongozo wa wewe kufikia mafanikio yako.


Watu waliofanikiwa wamejenga tabia ya kujiwekea malengo stahiki pamoja na mikakati ya kuyatimiza. Kila mara wanahakikisha wanafanya jambo kufikia au kuendeleza lengo lao.


Ni muhimu kufahamu kuwa lengo ni matokeo ambayo mtu anataka kuyafikia katika kipindi fulani cha muda; hivyo ni muhimu kubainisha matokeo hayo pamoja na njia utakazotumia ili kuyafikia.


6. Wanasoma sana


“Kusoma ni zana ya msingi katika kuishi maisha mazuri.”


Joseph Addison


Watu wengi hasa waafrika hawapendi kusoma. Watu husoma ikiwa kuna mitihani au kitu kingine cha lazima sana.


Watu waliofanikiwa wanasoma vitabu na makala nyingi kila mara kadri wanavyoweza. Mfano mzuri ni bilionea Bill Gates na Mark Zuckeberg, hawa wamekuwa mabalozi wakubwa wa vitabu pamoja na kuwahamasisha watu kusoma vitabu.


Kuna maarifa na hekima kubwa sana iliyofichwa kwenye vitabu; hivyo ni muhimu kujiwekea utaratibu wa kusoma vitabu na makala mbalimbali kama hii unayoisoma kutoka Fahamuhili.com.


Epuka au punguza kusoma vitu visivyo na tija kama vile udaku na maswala ya burudani.


7. Wanathubutu


Watu wengi wana mawazo mazuri lakini wana hofu na wasiwasi wa kuyafanyia kazi mawazo yao. Hali hii ni kinyume kwa watu waliofanikiwa kwani wao hufanya juu chini ili kufanyia kazi mawazo yao.


Hawaogopi kushindwa wala kupata hasara. Hivyo ikiwa tunataka kufanikiwa, ni lazima tuwe na udhubutu na ujasiri wa kufanya mambo.


“Ndoto zetu zote zinaweza kutokea ikiwa tuna ujasiri wa kuzifuata.”


Wale Disney


8. Wanalinda afya zao


Afya njema ndiyo msingi wa mafanikio yetu. Kamwe hatuwezi kuzalisha au kufanya kazi yoyote yenye tija ikiwa hatutakuwa na afya njema.


Watu waliofanikiwa wamejijengea utamaduni wa kukagua afya zao pamoja na kufanya mambo mbalimbali ili kuzilinda.


Ni muhimu kuhakikisha tunafanya mazoezi, tunakula chakula bora pamoja na kufanya uchunguzi wa kitabibu kila tupatapo nafasi.


9. Wanajali muda


Kutokujali muda ni tatizo linalowakabili watu wengi. Kutokana na kukosa utaratibu mzuri wa kutekeleza majukumu, watu wengi hupoteza muda kwenye mambo ambayo hayana maana.


Watu waliofanikiwa wana ratiba iliyopangiliwa vizuri na wanayoifuata kila siku. Hawatawaliwi na mambo kama vile sherehe, mitandao ya kijamii, starehe, marafiki, michezo n.k.


10. Wanajenga mahusiano


Siri nyingine ya mafanikio inayofahamika vyema kwa watu waliofanikiwa, ni kujega mtandao (network) wa mahusiano na watu sahihi. Ili kukamilisha lengo au maono yako ni lazima utahitaji watu fulani kwa namna moja au nyingine.


Hivyo ni muhimu kujenga mtandao wa mahusiano na watu sahihi ambao watakuwezesha kwa njia moja au nyingine kufikia lengo lako.


Hapa namkubuka blogger na marketer maaraufu Neil Patel, anaeleza kuwa kwa njia ya kujenga mahusiano na watu wakubwa ameweza kupata kazi kubwa zenye pesa nyingi.


Hitimisho


Naamini sasa hutoota tena mafaniko bali utaanza kuyatengeneza na kuyaishi. Ni wazi kuwa ili tuweze kufanikiwa ni lazima tuwe na tabia kama za watu waliofanikiwa. Je una tabia tajwa hapo juu?

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad