10/06/2020

Taharuki! Mafuvu ya Watu 6 wa Familia Moja Yakutwa MlimaniMABAKI ya mafuvu na miili ya watu sita wa familia moja wakazi wa Kijiji cha Kakese Mbugani wilaya ya Mpanda mkoan Katavi, waliopotea katika mazingira ya kutatanisha miezi miwili iliyopita, imeokotwa maeneo ya milimani ambako wananchi huwa wanafanya shughuli ya kuchimba mawe na kokoto.


 


Familia hiyo ilipotea miezi miwili iliyopita huku ndugu jamaa na marafiki kwa kushirikiana na mamlaka husika, walifanya jitihada za kuwatafuta bila mafanikio jambo ambalo lilileta hofu kubwa kwa wakazi wa kijiji hicho.


 


Wananchi waliendelea kufanya uchunguzi na kuikuta miili hiyo mlimani na waliweza kuzitambua nguo za marehemu ambazo walikuwa wakizivaa wakati wa uhai wao.


 


Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Benjamini Kuzaga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watu waliohusika na mauaji hayo ya kikatili.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger