10/12/2020

Tanzania yapokea kichapo kutoka kwa BurundiTimu ya taifa ya soka ya Tanzania, imekubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Burundi kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam

Tanzania ilikosa nafasi kadhaa kipindi cha kwanza na cha pili kupitia kwa nyota wake Simon Msuva, Mbwana Samatta na wengine kabla ya Burundi kutumia nafasi.

Dakika ya 80 kiungo wa Tanzania na klabu ya Simba Jonas Mkude alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na majizano na mshambuliaji Saido Berahino.

Dakika ya 86 mshambuliaji wa Burundi Saidi Ntibazonkiza akaifungia goli timu yake ambalo limedumu mpaka dakika 90 zinamalizika

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger