Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Trump na Obama warushiana vijembe wakati wa mkutano wa kampeni

 


Katika kampeni za Democratics anayewania nafasi ya urais akiwa Joe Biden huko Pennsylvania, Bwana Obama alimuhusisha Trump na mjomba ambaye amechanganyikiwa na kusema kuwa ana ubaguzi wa rangi.

North Carolina, katika kampeni za Republican rais alimkebehi Obama kwa kukosea katika uchaguzi wa mwaka 2016 .


Huku siku 13 zikiwa zimesalia kufikia siku ya uchaguzi ,Bwana Biden anaonekana bado anaongoza katika kura za maoni.


Lakini ni kiwango kidogo sana kwa mapendekezo hayo kuwa uhalisia, matokeo ya kuamua nani atakuwa rais yatajulikana Novemba 03.


Wamarekani wengi wanaonekana kuwa wanapiga kura ya maoni kwa wingi mwaka huu, mpaka sasa tayari kura milioni 42 za maoni zimepigwa.


Alisema ni maamuzi ya wapiga kura kuchagua kati ya "Trump ili wapone kabisa " au "Biden waingie kwenye msongo wa mawazo".


Bwana Biden alipumzika wiki nzima kwa ajili ya kujiandaa na majadala wa mwisho wa marais utakaofanyika usiku wa Alhamisi huko Nashville, Tennessee, wakati Trump akiwa anaendelea na kampeni katika majimbo ya pembezoni.


Rais hakusita kuingilia kati kampeni aliyoifanya Obama, kwa mara ya kwanza tangu kampeni hizo zianze mwezi Agosti.


"Hakukua na mtu yeyote ambaye alifanya kampeni kubwa kama Hillary Clinton zaidi ya Obama, si ndio?" Bwana Trump aliwaambia walioshiriki mkutano huo, alikuwa kila mahali.


Rais aliongeza: "Nadhani mtu ambaye hakuwa na furaha wakati Hillary aliposhindwa alikuwa Barack Hussein Obama."


Bwana Trump alimkejeli tena Obama kusema kuwa Bwana Biden hakuwa na vigezo vya kuwa rais, alipokua makamu wa rais mwaka 2009-2017.


Mwaka 2016, Bwana Obama aliripotiwa kuwa alimweka kando Biden kuwania nafasi ya urais na kumpa nafasi Hillary Clinton akiamini kuwa alikuwa anaweza kumshinda Trump.


Mwaka jana Obama alisema kuna uhitaji wa kuwa na mtu mpya katika uongozi wa Democratic, taarifa ambayo ilitafsiriwa kuwa hamkubali Biden.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments