.

10/24/2020

Tundu Lissu "Ni Kweli Nina TIKETI ya Kwenda Ubelgiji 18 December"

 


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amethibitisha kuwa, ni kweli ana tiketi ya ndege ya kuondoka nchini Desemba 18, 2020 kwenda Ubelgiji


Lissu amesema ataenda kutokana na matatizo ya kiafya aliyoyapata baada ya kupigwa risasi mwaka 2017, ambapo daktari wake amemuambia Desemba 20 arudi Ubelgiji ili aangalie maendeleo yake


Lissu mesema hayo akimjibu Mgombea wa Urais kupitia CCM, Dkt. John Magufuli ambaye alisema ana taarifa kuna baadhi ya wagombea wana tiketi za ndege ili wakimbie wakisababisha fujo nchini

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger