Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Ujumbe wa Zamaradi Kwenda Kwa Wema Sepetu "Bila Wewe Tusingejua Mambo ya Teams Tanzania"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Ujumbe mzito wa Zamaradi Mketema kuhusu Wema Sepetu


''I know unakuwa Excited kiasi gani linapokuja swala la Birthday yako, Just CELEBRATE, Una haki zote za kucelebrate.. Alama yako ni kubwa ulioiacha, sizungumzii ndani ya moyo wangu sababu hayo nishazungumza sana, lakini kwa WATANZANIA

Nyota yako imekuwa iking’aa tangu utambulishwe kwenye ulimwengu huu, na bado inaendelea kung’aa mpaka leo hii.. haijalishi inatoa mwanga wa namna gani.. ninachojua Inang’aa tu na kuendelea kumulikia wengi.. Umefanya mengi yanayopendeza na yasiyopendeza kama binaadamu wengine, lakini yote ndio yaliyomtengeneza Wema huyu tunaemuona leo, lakini katika yote yaliyotokea kwenye maisha yako, Nilichogundua ni kimoja tu.. UNAPENDWA MNO!!! Na ukitaka kujua mtu anapendwa kiasi gani, ni pale anapofanya kinyume na matarajio ya watu na bado akapata Support yao.. UNAPENDWA WEMA!! Na rekodi yako haijawahi kuvunjwa mpaka sasa tunapoongea, BADO!! na ndio hiyo ALAMA NINAYOIZUNGUMZIA..

Wewe ni ya aina ya wale watu ambao hata ajisaidie mchana kweupe uwanjani watu watakutetea watasema ulibanwa ungefanyaje, Jua sio kila mtu anapata hiyo Bahati, una watetezi wengi usiowajua, mawakili wengi usiowajua, wazungumzaji wengi usiowajua, wapenzi wengi mno usiowajua, tena wa nafasi na kaliba tofauti, na wote wanafanya kwa kujitolea Out of LOVE na si vinginevyo, kiufupi hauna baya kwa Watanzania, na bila wewe leo tusingejua mambo ya TEAMS Tanzania, tena Team iliyojitengeneza tu bila kikao, ikajikuta nguvu ya upendo imewakusanya kutoka pande tofauti za Dunia na wakawa kitu kimoja

Nataka nikukumbushe katika miaka yako 30 uliyoishi Duniani.. Uihesabu hiyo kama BARAKA YAKO KUBWA katika zile nyingi ambazo MUNGU amekubariki nayo, You a loved, Na kwakuwa sio kitu kinachonunulika kwa pesa means YOU ARE SPECIAL, sababu hata uwe na pesa kiasi gani hukiokoti tu, so please Dont take it for Granted

Baada ya maneno mengi acha niseme Happy Birthday to You TANZANIAN SWEETHEART.. Live Long Mamaa!! Na mimi binafsi nikiri.. NAKUPENDA Wema Sepetu''

Post a Comment

0 Comments