Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Ukipoteza Pasi Yanga Faini, Kaze Apiga ‘Stop’ Chips



INAELEZWA kuwa, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amewaam-bia wachezaji wa kikosi hicho kuwa makini wawapo mazoezini na kwenye mechi kwani akitokea mtu amepoteza pasi kizembe, basi huenda akapigwa faini.

Kaze raia wa Burundi, ameanza kuinoa Yanga Jumamosi iliyopita akichukua mikoba ya Zlatko Krmpotic raia wa Serbia ambaye ametimuliwa Oktoba 3, mwaka huu.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, Kaze ambaye ni muumini mkubwa wa soka la kasi na pasi nyingi, amewaambia wachezaji wake kuwa makini wawapo uwanjani kwa lengo la kumiliki sana mpira na kutowapa nafasi wapinzani kutawala mchezo.

“Kocha anataka kuona falsafa zake zinafanikiwa, hivyo basi amewaambia wachezaji kuwa makini katika kumiliki mpira na wasipoteze kirahisi.

“Atakayebainika kupoteza mipira kirahisi basi atapigwa faini ingawa mwenyewe hajaweka wazi hiyo faini ni kiasi gani,” alisema mtoa taarifa huyo.

Katika hatua nyingine, uongozi wa Yanga hadi jana jioni ulikuwa ukihangaika kusaka vibali vya kazi kwa ajili ya kocha wao huyo raia wa Burundi ili leo Alhamisi akae benchi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments