Vumbi la China lazua gumzo Korea Kaskazini, raia watakiwa kubaki ndaniKorea Kaskazini imetahadharisha raia wake kusalia majumbani kutokana na hofu ya ”vumbi la njano” linalopepea kutoka China kuwa linaweza kubeba virusi vya Corona


Taarifa ya KCTV kuhusu vumbi la manjano


Mitaa ya mji mkuu Pyongyang iliripotiwa kuwa mitupu siku ya Alhamisi baada ya tahadhari hiyo kutolewa.


Nchi hiyo ambayo imedai kuwa haina maambukizi ya virusi lakini imekuwa kwenye tahadhari kubwa tangu mwezi Januari, huku ikifunga kabisa mipaka na kuzuia mizunguko ya watu.


Hakuna uhusiano kati ya msimu wa mawingu ya msimu wa vumbi na Covid-19.


Hatahivyo, Si nchi pekee kudai uwepo kwa uhusiano huo. BBC imebainisha kuwa Turkumenistan pia imedai uwepo wa virusi kwenye vumbi ndio sababu raia wametakiwa kuvaa barakoa. Wamekataa kuwa walijaribu kuficha mlipuko huo.
‘Kuingia virusi hatari’


Televisheni inayodhibitiwa na serikali ya Korea (KCTV) ilitangaza kipengele cha taarifa ya hali ya hewa siku ya Jumatano , ikitahadharisha kuingia kwa vumbi la njano siku inayofuata. Ilitangaza pia marufuku ya kazi za ujenzi wa nje.


Vumbi la manjano linahusu mchanga kutoka jangwa la Mongolia na China ambalo hupiga Korea ya Kaskazini na Kusini wakati fulani wa mwaka. Imeingiliwa na vumbi lenye sumu ambayo kwa miaka imeibua wasiwasi wa kiafya katika nchi zote mbili.


Balozi pia ziliripoti kupokea onyo kuhusu wasiwasi wa vumbi la Pyongyang.


Ubalozi wa Urusi huko Pyongyang umesema katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imeionya pamoja na ofisi nyingine za kidiplomasia na mashirika ya kimataifa nchini humo kuhusu dhoruba ya vumbi ikiwataka wageni wote kubaki nyumbani na kufunga madirisha yao vizuri siku ya Alhamisi.


Wingi la vumbi linaweza kuwa na virusi vya Covid-19 ?

Kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani kimesema kuwa virusi vya Corona vinaweza kubaki kwenye ”hewa kwa saa kadhaa”. Hatahivyo, kimesema ni nadra sana mtu kupata maambukizi kwa njia hiyo- hasa nje. Njia pakee ni kuwa karibu na mtu aliye na maambukizi anayekohoa, kuoiga chafya au kuzungumza , na kusambasa kwa njia ya kutoa matone ya mate au mafua.


Vyombo vya habari nchi jirani ya Korea Kusini pia vimepinga mawazo hayo na kusema haiwezekani kuwa vumbi la manjano kutoka China linaweza kusambaza ugaonjwa wa Covid-19 kuelekea Korea Kaskazini. Kwa mujibu wa NK News.


Licha ya kudai kuwa nchi hiyo haina maambukizi ya ugonjwa wa Corona, kuna hofu kubwa huko Korea Kaskazini na kiongozi Kim Jong-un amekuwa akifanya mikutano ya hali ya juu kuhakikisha masharti makali yanatekelezwa.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE