Wabunge Kenya kuchukua likizo fupi kurekodi video ya wimbo 'Jerusalema'

Wabunge nchini Kenya wiki ijayo watachukuwa mapumziko mafupi kwenda kurekodi video ya densi ya Jerusalema maarufu kama #JerusalemaDanceChallenge ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Wimbo wa Jerusalema uliombwa na mwanamuzi wa Afrika Kusini Master KG umechochea kutengenezwa kwa video nyingi kote duniani.


Kiongozi wa walio wengi wa bunge la Kenya, Amos Kimunya, amenukuliwa akisema Spika na wakuu wote wa kamati za idara mbalimbali wataongoza wabunge wengine katika densi hiyo.


Alisema video hiyo itaangazia kazi za bunge na kuonesha umoja na waathirika wa janga la virusi vya corona.


Jennifer Shamalla, mbunge aliyeteuliwa, ametuma video kwenye mtandao wa Twitter inayoonesha wabunge wenzake wakifanya mazoezi.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE