10/21/2020

Wafanyabiashara Ubungo watolewa hofu kuhamia Mbezi

  


Meneja Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo, Maira Mkama, amewatoa hofu wafanyabiashara wa kituo hicho katika suala la kuhamia katika stendi mpya ya mbezi na kusema taratibu zikikamilika basi watakuwa kipaumbele kupata nafasi ya biashara kwenye kituo hicho.

 

Akizungumza na kurasa hii leo Meneja huyo amesema tayari serikali imetangaza kutafuta  mzabuni na kwamba baada ya kupatikana taratibu zingine zitafuata kwa wafanyabiashara watakaokidhi vigezo vilivyowekwa ili wapewe maeneo ya kufanyabiashara zao kwenye kituo hicho.


Meneja huyo ameongeza kuwa kila mwananchi ana haki ya kufanya biashara katika eneo hilo ambapo  amewatoa hofu wafanyabiashara hao na kudai kuwa hakuna mgogoro wowote utakaotokea kutokana na utaratibu mzuri uliowekwa ili kugawa maeneo ya kufanyiabiashara katika eneo hilo

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger