Wanamgambo wawaachilia huru Mfaransa na mwanasiasa waliokuwa wamewateka nyara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Sophie Pétronin, 75, alitekwa nyara nchini Mali Desemba 2016Image caption: Sophie Pétronin, 75, alitekwa nyara nchini Mali Desemba 2016

Familia ya raia wa mwisho wa Ufaransa aliyetekwa nyara na wanamgambo wa Kiislamu nchini Mali imesema ameachiliwa huru.


Familia hiyo imethibitisha Sophie P̩tronin Рmwenye umri wa miaka 75, mfanyakazi katika shirika la kutoa msaaada Рyuko njiani anaelekea mji mkuu wa Bamako РIngawa serikali ya Ufaransa bado haijathibitisha hilo.


Bi. Pétronin alitekwa nyara na kundi la kigaidi la al-Qaeda- lenye kuhusishwa na wanaume wenye silaha kaskazini mwa mji wa Gao ambako amekuwa akiendesha shirika la kutoa msaada.


Soumaïla Cissé alitekwa nyara akiwa kwenye msafara wa kampeniImage caption: Soumaïla Cissé alitekwa nyara akiwa kwenye msafara wa kampeni


Taarifa huko Mali zinasema kwamba raia mwingine aliyeshikwa mateka mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa mgombea urais Soumaïla Cissé, 70, pia nae ameachiliwa huru na wanamgambo hao.


Mwanasiasa huyo amekuwa akizuiliwa tangu mwezi Machi.


Inasemekana kwamba kuachiliwa kwao huru ni sehemu ya makubaliano yanayojumuisha kuachiliwa huru kwa wapiganaji wa jihadi zaidi ya 100 na mamlaka.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad