10/09/2020

Wanasiasa Pambaneni na Mambo ya SiasaMKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewaonya viongozi wa vyama vya siasa nchini wanaoingiza vijana kwenye mambo ya uhalifu kuendelea kupambana na siasa na si uhalifu.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, IGP Sirro, amesema kuwa uhalifu hauwezi kuwafanya wao kuwa viongozi huku akidai kuwa uwepo wa baadhi ya wananchi wachache walioandaliwa kufanya vurugu.

“Niwaombe sana wanasiasa pambaneni na mambo ya siasa msijaribu kuingiza vijana kwenye mambo ya uhalifu, uhalifu hauwezi kukufanya ukawa kiongozi sanasana mnawaharibia vijana maisha yao, maarifa yao, mwisho wa siku wanapata adhabu wanafungwa wanaacha familia zao” alisema IGP Sirro.

“ Niwaombe sana pambaneni na siasa muweze kuwa viongozi lakini msitiumie vijana kuwaingiza kwenye uhalifu wakipata shida na familia zao wakati nyinyi mnaenjoy maisha na familia zenu,” aliongeza IGP Sirro.

Aidha IGP Sirro amewaasa vijana kutokukubali kutumika vibaya na viongozi wa siasa badala yake wawaache wafanye uhalifu wenyewe ili wapambane na sheria zilizopo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger