10/05/2020

Waziri mkuu wa Japan Suga ashtumiwa kwa kukataa wasomi kujiunga na bodi ya ushauriWaziri mkuu mpya wa Japan Yoshihide Suga anakabiliwa na shtuma kwa kukataa wasomi sita kujiunga katika uanachama wa bodi ya ushauri wa kisayansi iliyoanzishwa baada ya vita vya pili vya dunia hatua ambayo wakosoaji wanasema inakiuka kanuni ya kikatiba ya uhuru wa kielimu. 

Suga aliyechukuwa hatamu za uongozi mwezi uliopita baada ya kujiuzulu kwa Shinzo Abe, amefurahia uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa wapiga kura wanaokubali ahadi zake za kupunguza sheria, kupunguza ada za simu za rununu na kutolewa kwa huduma kwa mfumo wa kidigitali anapojaribu kufufua uchumi na kukabiliana na janga la virusi vya corona.


 Lakini hatua ya Suga ya kuwakataa wasomi hao sita ambao baadhi yao wanajulikana kwa kukosoa sera za zamani za Abe inaweza ikazuia ghadhabu itakayomgonganisha na wapiga kura. 


Asilimia hamsini ya wanachama wa baraza hilo huchaguliwa baada ya kila miaka mitatu.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger