10/22/2020

Waziri wa Afya wa Ujerumani akutwa na virusi vya corona

 


Waziri wa Afya wa Ujerumani, Jens Spahn amethibitishwa kukutwa na #CoronaVirus na tayari ameshajitenga huku watu aliokutana nao wakijulishwa kuhusu hali yake

Spahn ni mmoja kati ya wanasiasa wakubwa wa Ujerumani kukutwa na Virusi hivyo. Uwiano wa maambukizi ya #COVID19 umefikia watu 50 kati ya 100,000


Ujerumani imerekodi visa 11,287 ndani ya saa 24 zilizopita na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 391,355 na vifo 9,999 hadi sasa


Idadi ya visa hivyo ni kubwa kurekodiwa tangu kuingia kwa maambukizi nchini humo ambapo kwa wiki za hivi karibuni nchi hiyo imeaza kurekodi maambukizi mapya kwa kasi

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger