10/16/2020

Wcb Wakimbiza Wasanii YoutubTakwimu zilizotolewa na matandao wa YouTube zinazohusisha channel za wanamuziki nchini Tanzania zilizotazamwa kwa wingi mwezi Septemba zimewaweka kileleni wasanii wa lebo ya WCB (Wasafi Classic Baby).


 


Katika kinyan’ganyiro hicho wasanii watano wa WCB wameingia 10 bora huku nafasi ya kwanza mpaka ya nne ikishikiliwa na wasanii hao.

Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’ ameshika nafasi ya kwanza channel yake kutazamwa na watu milioni 27.2, Zuchu ameshika nafasi ya pili channel yake ikitazamwa na watu milioni 19.5, Ray Vanny amekamata nafasi ya tatu channel yake ikitazamwa na watu milioni 15.6.Wasanii wengine wa WCB walioingia katika 10 bora ni Mbosso aliyeshika nafasi ya tano channel yake ikitazamwa na watu milioni 7.6 huku Lavalava akishika nafasi ya saba kwa channel yake kutazamwa na watu milioni 4.2 na kufanya listi ya wasanii WCB kufikia tano.

Aidha, wakali wengine watano bongo walioingia 10 bora ni Harmonize (4), Alikiba(6), Aslay(8), Nandy(9) na Jux(10).


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger