10/14/2020

Wema Sepetu, Kajala Masanja Wakikutana ni Umbea Kama Wote Kwa Kwenda MbeleMALKIA wa fi lamu za Kibongo, mwenye jina kubwa ndani na nje ya Bongo, Wema Isaac Sepetu amesema kuwa, yeye na staa mwenzake, Kajala Masanja walikuwa na umbeya mwingi kama wote wa kuzungumza na mpaka sasa bado hawajaumaliza.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Wema alisema kuwa, mara nyingi mnapokuwa marafi ki, mnakuwa na umbeya mwingi wa kuzungumza hivyo kitendo cha kukaa miaka mitano bila kuzungumza walimisi vingi hivyo sasa hivi wakikutana wanakuwa hawamalizi yote.


“Unajua mimi na Kajala, japokuwa tuligombana, lakini ukweli ni kwamba tulikuwa na vitu vingi sana vya kuongea wakati tulipokuwa marafi ki hivyo tulivyopatana, bado hatujamaliza, kila siku tunaongea kidogokidogo,” anasema Wema huku akicheka.


Wema na Kajala waligombana takriban miaka mitano iliyopita, chanzo cha ugomvi wao kikidaiwa ni mwanaume japokuwa wawili hao wamesaidiana kwenye vitu vingi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger