Wizara ya Elimu yafuta Mtaala wa Ualimu ngazi ya cheti

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza kufuta mtaala wa ualimu wa ngazi ya cheti kwa elimu ya awali na msingi ikiwa ni hatua ya kuboresha elimu nchini.

Kwa mujibu taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia inasema hatua hiyo inakwenda sambamba na kufanyia kazi maoni ya wadau ambao wamekuwa wakiyatoa likiwemo la kufuta mtaala huo.


Taarifa hiyo inasema mtaala ulioboreshwa unatoa nafasi kwa mwalimu katika mwaka wa pili wa masomo kuchagua eneo la umahiri atakalobobea tofauti na mfumo wa zamani ambao haukuwa katika muktadha huo.


Mtaala huu mpya utaanza kutumika katika mwaka wa masomo 2020/21 na kwamba mwalimu yeyote mwenye cheti cha ualimu atakuwa na sifa ya kusomea Diploma ya 


ualimu wa elimu ya awali au msingi na vilevile atakapohitimu na kufaulu atakuwa na sifa ya kujiunga na Chuo Kikuu kupata Shahada ya kwanza ya ualimu wa elimu ya awali au msingi.


Programu itakayofundishwa itakuwa ya miaka mitatu na kwamba masomo 


yatafundishwa kwa lugha mbili ambazo ni Kiingereza na Kiswahili kutokana na kuwepo kwa shule za English medium nchini.


Walimu waliosoma Astashada (CHETI) bado Serikali inatambua Uhitimu wa cheti katika kada ya ualimu na ipo kwenye mfumo wa utumishi na itaendelea kuwepo na hakuna mwalimu atakayefukuzwa kazi kwa kuwa yeye ni mwalimu wa ngazi ya cheti.


Kwa walimu walioko kazini watakaopenda kujiendeleza wanaweza kusoma kwa masafa kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania(TIE) kwa njia ya masafa, njia ambayo haita athiri 


utendaji na mwisho kufanya mitihani ili kupata Diploma. 


Kwa walimu ambao wana 


vyeti na hawajaweza kupata fursa ya ajira, watatakiwa kurudi vyuoni na kuweza kupata Diploma ya ualimu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad