10/07/2020

Zitto Kabwe apata ajali mkoani KigomaChama cha ACT-Wazalendi kimeeleza kuwa kiongozi wa chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe amepata ajali ya gari akiwa njiani akitokea Kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika Jimbo la Kigoma Kusini


Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari iliyotolewa na Afisa Habari ACT-Wazalendo, Arodia Peter, ilieleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana ambapo Zitto alikuwa na watu watano kwenye gari yake.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo Zitto na watu hao ote wako salama ingawa walipata majeraha na wanahisi maumivu makali.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba baada ya ajali hiyo walipata huduma ya kwanza kwenye eneo la ajali baadaye walipelekwa Kituo cha Afya cha Kalya kilichopo Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger