10/18/2020

Zuchu: Ni kweli Ninabebwa!

 


STA A wa Bongo Fleva anayefanya poa kwa sasa na memba wa lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman ‘Zuchu’, amefunguka kuwa, ni kweli anabebwa na lebo, maana ni kawaida kwa msanii yeyote aliye chini ya menejimenti.

Zuchu ambaye kwa sasa anakimbiza na ngoma zake ya Cheche na Litawachoma, ameiambia IJUMAA SHOWBIZ kuwa, hiyo ndiyo kazi ya lebo maana hata wanamuziki wakubwa kama Rihana waliwekewa mazingira kama yeye.

“Wanaosema nabebwa na lebo walitaka iweje? Maana ni kawaida kwa msanii kubebwa na lebo na duniani kote kitu hicho kipo na hii inakuwa ni promosheni kwa msanii.

“Wanamuziki wakubwa duniani wanafanyiwa hivyo, Watanzania wanatakiwa wajue ni kazi ya lebo kumbeba msanii na kumfikisha pakubwa na ningekuwa sibebeki, nisingekuwa hapa kwa sababu nimevumilia mengi na nisingekaa bure kwa muda wote huo,’’ amesema Zuchu.


STORI: HAPPYNESS MASUNGA

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger